Tovuti ya TACAIDS  inalenga  kusambaza taarifa muhimu za  VVU na UKIMWI kwa jamii, pamoja na kubadilishana uzoefu na wadau wanao tekeleza afua za UKIMWI nchini, ili kuboresha mapambano ya UKIMWI na kufikia malengo yetu ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi ya VVU.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Leonard L. Maboko
MKURUGENZI MTENDAJI

Sekretarieti za Mikoa (RSs) zimepewa jukumu la uratibu, usimamizi na kurahisisha kazi kwenye wilaya na jamii.

Kuundwa kwa Wakala za Uwezeshaji za Mikoa. (RFAs), kila moja ikiwakilisha mikoa miwili ilikuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha msaada wa kiufundi na kifedha unaotolewa wilayani na kwenye jamii. RFAs zinaonekana kama macho, masikio na mikono ya TACAIDS. Ziliweza kuchochea kwa kiasi kikubwa, mwitikio wa wilayani kupitia kujenga uwezo na kuelekeza fedha kwenye CSOs. Pia zimekuwa zikitoa msaada wa kiufundi kwa RSs na CMACs. Hata hivyo RFAs zimekuwa changamoto kubwa katika kufikia na kutoa huduma katika mikoa miwili inayoshughulika nayo. Hili lilikuwa tatizo lililosababisha changamoto kwa upande wa ununuzi na usafirishaji, kudhibiti muda na utoshelevu wa rasilimali. Zaidi ya hayo, kutokana na kwamba RFAs hazikuwa kwenye muundo wa serikali, ilisababisha wakati mwingine kutiliwa shaka na wadau katika ngazi ya mikoa na hivyo kuonekana kama chombo mbadala au pinzani. 

Kuanzishwa kwa shughuli za UKIMWI wilayani, vijijini, na kata kunahitaji rasilimali endelevu kwa upande wa mafunzo, usimamizi na msaada wa kiufundi. Matumizi ya Kanuni ya Dhana Tatu katika ngazi ya wilaya yameonyesha kuwa changamoto kubwa kwa watendaji wote kutokana na kukosa uzoefu katika mipango shirikishi na uunganishaji pamoja na kuchangia majukumu baina ya sekta mbalimbali. Ushirikishaji wa CSo, katika mipango ya halmashauri unahitaji kuimarishwa, wakati kuaminiana na kusaidiana miongoni mwa watendaji mbalimbali kunahitaji kuendelezwa. 

Katika ngazi ya jamii, kuna maelfu kadha ya mashirika ya kijamii (CBOs), pamoja na Mashirika ya Dini (FBos). Hivi vimetoa mchango mkubwa katika Mwitikio wa Taifa, hasa mahali ambapo kulikuwa na fedha na msaada wa kiufundi kupitia asasi zisizo za serikali (AZISE). Nyingi za asasi hizi pia zinajihusisha na ART. Pamoja na idadi yao, uwezo na ubora wa huduma na afua zinazotolewa na CBOs hizo vinatofautiana sana. Uzingatiaji wa miongozo mizuri na ushirikishaji katika jamii pamoja na mipango ya wilaya ni changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi.