Tovuti ya TACAIDS  inalenga  kusambaza taarifa muhimu za  VVU na UKIMWI kwa jamii, pamoja na kubadilishana uzoefu na wadau wanao tekeleza afua za UKIMWI nchini, ili kuboresha mapambano ya UKIMWI na kufikia malengo yetu ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi ya VVU.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Leonard L. Maboko
MKURUGENZI MTENDAJI

Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) 

 

Masuala ya Kimkakati: 

Hakuna sera mahususi kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI. Wengi wa watu walioambukizwa Virusi vya UKIMWI (kiasi cha wanane kati ya kumi) hawajui kuwa wameambukizwa. Upataji fursa ya kupima, kuongezeka kwa dawa za kuongeza kinga ya mwili (ARV) na kuboreka kwa mwitikio wa mahitaji ya lishe kwa wanaotumia vidonge vya kuongeza kinga ya mwili, lazima vibadili hali hii. Wengi wa wale wanaokufa kwa maradhi yanayohusiana na UKIMWI hawatajua kwa uhakika kuwa wamekufa kwa UKIMWI, au wasingekiri kuwa yawezekana kuwa UKIMWI. Katika hali kama hiyo, kaya zilizoathiriwa hazitajiona kuwa zimeathiriwa moja kwa moja au kinyume chake na VVU na UKIMWI; bali ni kaya yenye umaskini unaoongezeka zaidi. Kutokana na maradhi sugu au vifo vya mapema mwitikio mpana wa maendeleo, unaoingia katika MKUKUTA, ni muhimu sana kwa suala hili.

 

Kwa wale wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (na wanaojua au kutuhumu kuwa na VVU) na familia zao, unyanyapaa na ubaguzi vitaendelea kuwakilisha changamoto muhimu kwa afya na maisha yao kwa miaka mingi ijayo. Masuala haya yanaweza kukabiliwa vizuri zaidi kwa njia ya unyanyapaa na ubaguzi, ingawa pia yanahitaji kuimarisha mitandao ya WAVIU. (Masuala haya yanashughulikiwa katika Eneo Lililodhamiriwa: Mazingira Wezeshi: Lengo la Kimkakati la 2: Kupambana na Unyanyapaa, Kujikataa na Ubaguzi).

 

Kadiri huduma za kupima zinavyoongezeka na watu wengi wanakwenda kupima, ongezeko la rufaa litatokea katika vyama imara vya baada ya kupima na WAVIU, vinavyohitaji msaada zaidi kutoka katika mitandao ya taifa. Bahati mbaya, mitandao hii bado ni dhaifu, kwa kiasi kikubwa kwa sababu inaundwa na wanachama wa aina nyingi wenye maslahi tofauti, pia ni kutokana na matatizo mengine ya muundo. Wengi wa wale wanaokwenda kupima wanafanya hivyo baada ya kuugua sana kwa muda, na baada ya kumaliza rasilimali, na wale wanaojua kuwa wana VVU na kutafuta msaada nje ya familia zao, wanaelekea kutoka katika kaya maskini.

Kwa baadhi ya WAVIU, njia zao za kuendeshea maisha zimeathiriwa sana, kwa kupoteza mtafutaji mkuu kumeathiri sana mikakati ya kuendeshea maisha. Kundi hili halina budi kulengwa kwa ajili ya msaada wa kiuchumi na stadi za kuboresha njia zao za kuendeshea maisha. Matokeo hayo huenda yakaathiri wanaume na wanawake kwa viwango tofauti.

 

Madhumuni ya Kimkakati: 

 

Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI (WAVIU) na wadau wengine wanawezeshwa kushughulikia ipasavyo mahitaji na haki za WAVIU, kwa kuzingatia hali mbalimbali na mahitaji ya wanawake na wanaume. 

 

Mikakati

 1. Kuhimiza uanzishwaji wa muungano imara wa vyama vya WAVIU katika ngazi ya taifa.
 2. Kutathmini mazingira ya sheria, kitaasisi, sera ya mkakati yanayoathiri WAVIU na mwitikio wa taifa, na kutoa mapendekezo kuhusiana na hayo.
 3. Kutafuta njia za kupanua fidia za bima kwa wale wenye Virusi vya UKIMWI katika sekta rasmi.
 4. Kusaidia utekelezaji wa Sheria ya VVU/UKIMWI kupunguza ubaguzi dhidi ya WAVIU.
 5. Kuimarisha sauti na ushawishi wa WAVIU, kuwa ndio wenye haki, katika maamuzi ya taifa yanayoathiri maisha yao, na maisha ya wengine, kujali kutambua kuwa wanawake na wanaume wana ushawishi tofauti mwanzoni.
 6. Kuimarisha taratibu za haki za binadamu ili zishughulikie zaidi mahitaji na matakwa ya WAVIU.
 7. Kuhusisha mamlaka za serikali za mtaa, vyama vya kiraia, jamii, na WAVIU wenyewe kama wabia muhimu katika kubuni, kupanga, kusaidia na kutathmini mikakati ya kijamii na mikakati mingine ya kusaidia WAVIU.
 8. Kutumia taratibu za kijamii na afua za vituo vya afya kubainisha na kusaidia rufaa za WAVIU walio hatarini zaidi na wagonjwa sugu wa muda mrefu.
 9. Kusaidia juhudi za kijamii kuongezea na kusaidia mahitaji ya ugavi wa chakula kwa WAVIU wenye shida, na kutafuta msaada wa ziada iwapo msaada wa lishe kwa wanaotumia vidonge vya kuongeza kinga ya mwili (ARV) hayatoshi.
 10. Kuongeza wanachama katika vyama vya WAVIU kuimarisha msaada wa hali na mali kwa wanaohitaji na kuimarisha wajibu wao katika uraghibishi na upunguzaji unyanyapaa.
 11. Kutumia taratibu za kijamii kuainisha na kusaidia rufaa za WAVIU wanaougua kwa huduma ya matibabu.
 12. Kutoa msaada wa kawaida (usio wa kitaalamu) wa saikolojia na jamii, uliolengwa kwa wale wanaohitaji zaidi.

Viashirio:

 1. Asilimia ya watu wanaoonyesha mtazamo wa kukubali watu wenye VVU.
 2. Kuwepo kwa muungano wa kitaifa wa vyama vya WAVIU wenye kuungwa mkono na vikundi vikuu vya msaada wa WAVIU nchini Tanzania.
 3. Asilimia ya vikundi vya msaada wa WAVIU vinavyofanya kazi (vinavyofanya kazi maana yake vikundi vya msaada wa WAVIU vinavyotoa stadi za namna ya kujiendeshea maisha, msaada wa kisaikolojia kwa wanachama wao, vinavyoweza kufanya shughuli za uraghibishi, vinavyoelewa programu za VVU za mahali pa kazi za kitaifa na vinaweza kuhimiza mafunzo yenye manufaa.