Tovuti ya TACAIDS  inalenga  kusambaza taarifa muhimu za  VVU na UKIMWI kwa jamii, pamoja na kubadilishana uzoefu na wadau wanao tekeleza afua za UKIMWI nchini, ili kuboresha mapambano ya UKIMWI na kufikia malengo yetu ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi ya VVU.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Leonard L. Maboko
MKURUGENZI MTENDAJI

Dira ya TACAIDS ni:

Tanzania inaendeleza juhudi za pamoja za kupunguza kuenea kwa VVU na kutoa matunzo bora zaidi kwa wale walioathirika na walioathiriwa na virusi.

Dhamira ya TACAIDS ni:

Kutoa mwongozo na kulinda uongezaji na upanuzi wa ubora wa kinga, matunzo na msaada dhidi ya VVU/UKIMWI na kuwa na ushawishi mkubwa kwenye programu na shughuli mbalimbali za kudhibiti na kupunguza athari ndani ya programu ya mwitikio shirikishi wa Taifa yenye uratibu mzuri unaongozwa na Serikali Kuu, kushikizwa kwenye Halmashauri za Serikali za Mitaa, kujikita ndani ya jamii na kusaidiwa na wadau wote wanaohusika.