Tovuti ya TACAIDS  inalenga  kusambaza taarifa muhimu za  VVU na UKIMWI kwa jamii, pamoja na kubadilishana uzoefu na wadau wanao tekeleza afua za UKIMWI nchini, ili kuboresha mapambano ya UKIMWI na kufikia malengo yetu ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi ya VVU.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Leonard L. Maboko
MKURUGENZI MTENDAJI

Kuacha

Baadhi ya balehe wanaweza kuhitaji taarifa kuhusu kuacha ngono na wengine wanaweza kutaka taarifa kuhusu kutumia kondomu kwa usahihi na mara kwa mara.

Kuwa mwaminifu

Vijana hawana budi kulea stadi za kukwepa hatari, kama vile ucheleweshaji wa kufanya ngono kwa mara ya mwanzo, kuacha, majadiliano na wenzi wa ngono na matumizi thabiti ya kondomu. Elimu ya VVU inapaswa ianze mapema, ikiwezekana kabla watu hawajaanza ngono. Kwa wale ambao wanafanya ngono, upunguzaji wa wenzi na matumizi thabiti ya kondomu ni muhimu sana. Vijana walio katika uhusiano thabiti wanahitaji kufahamu kwamba uaminifu wa pande zote mbili unalinda tu pale ambapo wenzi wote wawili wanapimwa na hawana VVU. Hivyo, kuwapa vijana maarifa na stadi za kujadili kuhusu masuala ya kingono, kufuata mitazamo na desturi zinazowalinda dhidi ya maambukizo ya VVU na kupata huduma za afya ya uzazi ni vipengele muhimu. Stadi za maisha na tabia ya uwajibikaji wa wanaume katika uhusiano wa kingono na kifamilia, ikiwa ni pamoja na utawala wa mwanamume, kuwa mzazi bila kujali majukumu, mnyanyasaji wa majumbani na wa kijinsia, vinahitaji kushughulikiwa kupitia stadi za maisha. Ni muhimu sana kuwa na majadiliano ya wazi kuhusu ujinsia wa ujana na kutokomeza welewa potofu kuhusu VVU.

Tumia kondomu

Baadhi ya wanaume wana wenzi wengi wanawake wa ngono na hili huwaweka wote katika hatari ya uambukizo ya hali ya juu. Wakiambukizwa wana uwezekano wa kusambaza virusi kwa wenzi wao wa ngono. Mara nyingi, baadhi ya wanaume hukataa kutumia kondomu na kutoa visingizio. Wengine wanapoambukizwa, huwalaumu wake zao visivyo haki kwa maambukizo hayo ili kuwanyamazisha. Katika hali kama hizo wanawake hawawezi kujibu kitu kwa sababu hawana stadi na uwezo wa kuwakabili wenzi wao. Utamaduni pia unawategemea kuvumilia lawama na kuonyesha heshima kwa wenzi wao kwa njia yoyote ile.