Tovuti ya TACAIDS  inalenga  kusambaza taarifa muhimu za  VVU na UKIMWI kwa jamii, pamoja na kubadilishana uzoefu na wadau wanao tekeleza afua za UKIMWI nchini, ili kuboresha mapambano ya UKIMWI na kufikia malengo yetu ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi ya VVU.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Leonard L. Maboko
MKURUGENZI MTENDAJI

IDARA YA URATIBU WA MWITIKIO WA TAIFA

Lengo Kuu

Kuratibu shughuli za watekelezaji wote wa masuala ya VVU na UKIMWI nchini Tanzania kupitia miundo iliyopo na kwa kuweka mifumo ya uratibu. 

Majukumu

 

 • Kuratibu shughuli zinazolenga kuimarisha mwitikio wa Taifa dhidi ya UKIMWI;
 • Kubuni programu za kujenga uwezo na kufuatilia utekelezaji wake;
 • Kutoa msaada wa kiufundi kwa watekelezaji wote wa masuala ya VVU na UKIMWI nchini kupitia ngazi ya mkoa;
 • Kuratibu shughuli za UKIMWI katika Sekta ya Umma, Sekta Binafsi; Asasi za Kiraia zikiwemo Asasi za Dini, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
 • Kujenga uwezo na kuimarisha mitandao mbalimbali na mashirika katika ngazi zote
 • Kuangalia shughuli zote zinazopendekezwa na ofisi za Mikoa

IDARA YA URAGHBISHI

Lengo kuu

Kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa mikakati ya uraghibishi kuhusu  UKIMWI  na wadau wote wa habari zinazohusiana na UKIMWI

Majukumu

 • Kuandaa programu za uraghibishi na kufuatilia  utekelezaji wake
 • Kuratibu shughuli za uraghibishi
 • Kutunza, kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka mbalimbali zinazohusu  UKIMWI pamoja na kutoa huduma za maktaba kwa wadau  na wananchi kwa ujumla.

IDARA YA SERA, MIPANGO NA UTAFITI

Lengo kuu

Kusimamia utekelezaji wa sera na kutoa miongozo ya utekelezaji wa mkakati wa taifa wa kudhibiti UKIMWI na utafiti kuhusu mwitikio wa taifa wa mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI nchini Tanzania.

Majukumu

 • Kuandaa mikakati ya utafutaji rasilimali fedha na matumizi yake
 • Kufanya utafiti kuhusu VVU/UKIMWI
 • Kuhimiza na kuwezesha huduma za sekta binafsi katika Tume
 • Kuhakikisha kuwa mipango na bajeti ya VVU/UKIMWI inajumuishwa katika mchakato wa bajeti ya serikali.

 

Idara hii ina sehemu tatu zifuatazo

 • Sera
 • Mipango na
 • Utafiti

 

KITENGO CHA UFUATILIAJI NA TATHMINI

Lengo Kuu

Kutoa utaalamu na huduma kuhusu ufuatiliaji na tathmini

Majukumu

 • Kuandaa mipango ya utekelezaji kuhusu VVU/UKIMWI
 • Kuandaa miongozo ya uoanishaji wa mifumo na mbinu za viashirio kwa ajili ya tathmini ya mipango na athari zake.
 • Kukusanya na kuchambua data kutoka kwa watekelezaji wa shughuli za VVU/UKIMWI nchini.
 • Kuchambua data za VVU/UKIMWI ili ziwe taarifa kwa watumiaji mbalimbali

 

IDARA YA FEDHA NA UTAWALA

Lengo Kuu

Kusimamia na kutoa utalaamu wa masuala yote ya fedha, utumishi na utawala katika Tume

Majukumu

 

 • Kutoa miongozo ya menejimenti ya masuala ya fedha kwa wadau wote wanaoshughulika na VVU na UKIMWI na     kufuatilia Utekelezaji wake;
 • Kusimamia utoaji wa ruzuku;
 • Kusimamia maendeleo ya rasilimali watu

Vitengo vingine ni kama vifuatavyo:

 1. Kitengo cha Menejimenti ya Mifumo ya Habari
 2. Kitengo cha Menejimenti ya Manunuzi
 3. Kitengo ch Ukaguzi wa Ndani
 4. Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
 5. Kitengo cha Huduma za Sheria
 6. Kitengo cha Programu Maalum