Tovuti ya TACAIDS  inalenga  kusambaza taarifa muhimu za  VVU na UKIMWI kwa jamii, pamoja na kubadilishana uzoefu na wadau wanao tekeleza afua za UKIMWI nchini, ili kuboresha mapambano ya UKIMWI na kufikia malengo yetu ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi ya VVU.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Leonard L. Maboko
MKURUGENZI MTENDAJI

Upunguzaji Athari

Watoto walio katika mazingira magumu:

Msaada wa jamii, kwa watoto walio katika mazingira magumu kupitia mwitikio shirikishi unaimarishwa na kusaidiwa na utoaji huduma zilizopanuliwa.

Walioathiriwa:

Uwezo wa watu binafsi, familia na jamii kushughulikia athari za VVU na UKIMWI unaimarishwa.

Watu wanaoishi na VVU na UKIMWI

Watu wanaoishi na VVU na UKIMWI (WAVIU) na wadau wengine wanawezeshwa kushughulikia ipasavyo mahitaji na haki kwa WAVIU kwa kuzingatia hali tofauti pamoja na mahitaji ya wanawake na wanaume.