Tovuti ya TACAIDS  inalenga  kusambaza taarifa muhimu za  VVU na UKIMWI kwa jamii, pamoja na kubadilishana uzoefu na wadau wanao tekeleza afua za UKIMWI nchini, ili kuboresha mapambano ya UKIMWI na kufikia malengo yetu ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi ya VVU.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Leonard L. Maboko
MKURUGENZI MTENDAJI

Kutokana na tulichojifunza kutoka kwenye vituo vya majaribio vilivyosimamiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na UNICEF, vituo vya utoaji wa huduma za uzuiaji wa Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto viliongezeka na kufikia 710 nchini ilipofika mwaka 2006. Karibu 12% ya kinamama wajawazito wanaopaswa kupata dawa za ARV walipata dawa hizo ili kupunguza maambukizo ya VVU kwa watoto wakati wa kujifungua. Miongozo ya kupunguza maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto (PMTCT) ilifanyiwa mapitio katika jitihada za kuhamasisha matunzo kamambe na matibabu kwa kinamama walioathirika.

Juhudi za kuenea kwa vituo vya huduma za kinga ya maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) nchini zimekuwa ndogo kutokana na muundo wa utoaji wa huduma hizi ambao kimpango husimamiwa na serikali kuu, upungufu wa dawa kutokana na kutokuwa na makadirio mazuri ya dawa na matatizo ya usambazaji wa dawa zenyewe, kuwepo kwa sera inayoruhusu kinamama wajawazito kupewa dawa za ARV kipindi cha mwisho cha ujauzito (kuanzia wiki ya 28) na ufuatiliaji hafifu wa mama na mtoto.