Tovuti ya TACAIDS  inalenga  kusambaza taarifa muhimu za  VVU na UKIMWI kwa jamii, pamoja na kubadilishana uzoefu na wadau wanao tekeleza afua za UKIMWI nchini, ili kuboresha mapambano ya UKIMWI na kufikia malengo yetu ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi ya VVU.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Leonard L. Maboko
MKURUGENZI MTENDAJI

Zifuatazo ni kazi za TACAIDS: -

 1. Kutunga miongozo kwa ajili ya mwitikio wa mapambano dhidi ya janga la UKMIWI na usimamizi wa athari zake Tanzania Bara
 2. Kutayarisha mkakati kwa ajili ya mipango na shughuli za udhibiti wa VVU/UKIMWI kwa mujibu wa mkakati wa Taifa.
 3. Kukuza uhusiano wa kitaifa na kimataifa miongoni mwa wadau wote kupitia uratibu bora wa mipango na shughuli zote za kudhibiti UKIMWI kwa mujibu wa mkakati wa Taifa.
 4. Kutafuta, kugawa kulingana na mahitaji na kufuatilia matumizi yake.
 5. Kusambaza na kubadilishana taarifa kuhusu janga la VVU/UKIMWI na madhara yake nchini Tanzania ili tuweze kudhibiti janga hilo.
 6. Kuhimiza na kuimarisha utafiti, ubadilishanaji taarifa na nyaraka na utunzaji kumbukumbu kwa ajili ya kuzuia na kudhibiti VVU/UKIMWI.
 7. Kuimarisha program za uraghbishi na elimu kwa kiwango cha juu.
 8. Kufuatilia na kutathmini shughuli zote za VVU/UKIMWI
 9. Kuratibu shughuli zote za kudhibiti janga la UKIMWI nchini Tanzania kwa mujibu wa mkakati wa Taifa.
 10. Kuwezesha juhudi za kupatikana tiba na chanjo na kuimarisha upatikanaji wa huduma na matunzo.
 11. Kuilinda haki za jamii ya watu walioathiriwa na walioathirika na VVU/UKIMWI
 12. Kujenga mazingira wezeshi kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI waweze kukubali hali
 13. Kuishauri serikali kuhusu masuala yote ya udhibiti wa VVU/UKIMWI Tanzania bara.
 14. Kubainisha vikwazo vya utekelezaji wa afua za VVU/UKIMWI katika sera za kinga, mipango na kuhakikisha ufikiwaji wa malengo yaliyowekwa.
 15. Kuimarisha shughuli zote zinazohusu huduma za kinga na udhibiti wa janga la UKIMWI katika yafuatayo:
 • Huduma za afya na ushauri kwa watu wanao ugua UKIMWI
 • Ustawi wa wafiwa, yatima na wategemezi waliobaki.
 • Kushughulikia masuala ya kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kisheria yanayohusu janga la UKIMWI
 1. Kutekeleza shughuli na majukumu mengine yeyote yanayohusu kinga na udhibiti wa UKIMWI katika Tanzania bara kama Tume itakavyoona inafaa.