Tovuti ya TACAIDS  inalenga  kusambaza taarifa muhimu za  VVU na UKIMWI kwa jamii, pamoja na kubadilishana uzoefu na wadau wanao tekeleza afua za UKIMWI nchini, ili kuboresha mapambano ya UKIMWI na kufikia malengo yetu ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi ya VVU.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Leonard L. Maboko
MKURUGENZI MTENDAJI

Matibabu ya Maradhi Nyemelezi pamoja na kutoa Dawa za Kuongeza Kinga ya Mwili

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetayarisha na inatekeleza mpango wa matibabu ya maradhi nyemelezi (OI) na utoaji wa Dawa za Kuongeza Kinga ya Mwili. Kulingana na mpango huu watu milioni 2 waliokuwa wanaishi na virusi vya UKIMWI kati ya karibu watu 400,000-500,000 walikuwa wanahitaji ARV, wakati watu milioni 1.2 walikuwa wanahitaji dawa za kutibu maradhi nyemelezi. Mwishoni mwa mwaka 2006 zaidi ya watu 70,000 walikuwa wanapata dawa za kuongeza kinga ya mwili kupitia hospitali za umma na binafsi, hili ni ongezeko kubwa la karibu watu 2000, kwa mwaka 2003. Ili kutekeleza ipasavyo Mpango wa Matunzo na Matibabu, Wizara imeimarisha vituo vya huduma za afya na ilitoa mafunzo maalumu kwa wataalamu wa Afya na imeanza kuajiri wafanyakazi wapya kupitia mpango wa dharura wa kuajiri watumishi wa sekta ya Afya.

 

Licha ya jitihada hizi, miundombinu ya afya kwa sasa imelemewa na uwezo wa kuhimili mahitaji ya ziada ya kutibu maambukizo nyemelezi na utoaji wa dawa za kuongeza kinga ya mwili. Mpango wa kupanua huduma za utoaji dawa za kuongeza kinga ya mwili haukusaidiwa na mawasiliano ya kutosha kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, watoa huduma na jamii kwa ujumla katika kuhamasisha mahitaji ya dawa hizo, kuhakikisha ufuasi wa masharti ya matumizi ya dawa, kulinda dhidi ya matumizi mabaya ya dawa hizo, kuwapo kwa kiwango kikubwa cha wagonjwa wenye kifua kikuu wenye virusi vya UKIMWI. Pia, ushirikiano kati ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma vya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika kutoa huduma za afya ni muhimu zaidi hivi sasa kuliko ilivyowahi kutokea.