Tovuti ya TACAIDS  inalenga  kusambaza taarifa muhimu za  VVU na UKIMWI kwa jamii, pamoja na kubadilishana uzoefu na wadau wanao tekeleza afua za UKIMWI nchini, ili kuboresha mapambano ya UKIMWI na kufikia malengo yetu ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi ya VVU.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Leonard L. Maboko
MKURUGENZI MTENDAJI

Kulingana na Kanuni ya Dhana Tatu, Tanzania imeendeleza na kuimarisha miundo ya asasi zake katika kuratibu Mwitikio wa Taifa. Katika ngazi ya taifa, kuanzishwa kwa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Wizara ya Kukabili Majanga na UKIMWI zilikuwa ni hatua dhahiri.Pia kuundwa kwa Kamati ya Ufundi ya Wizara mbalimbali kuhusu UKIMWI (IMTC) kumeongeza msukumo kwenye mwitikio wa UKIMWI nchini. TACAIDS imekuwa ni kiungo muhimu cha kitaifa. Tume hii imekuwa na kazi nyingi zinazoongezeka kila mara kama vile kutoa mwongozo na msaada wa kiufundi kwenye jamii na sekta binafsi nchini.

 

Ndani ya kazi hii ya kuongoza na kuratibu:

  • Wizara, Idara, Wakala na Mamlaka za Serikali za Mitaa zimeunganisha mipango ya afua pamoja na bajeti ambazo zimefungamanishwa kwenye MTEF kwa ajili ya programu muhimu za VVU mahali pa kazi katika shughuli muhimu za sekta.
  • Pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, mwitikio wa kigatuzi ulianzishwa kupitia Kamati za UKIMWI wilayani (CMAC), kata (WMAC) na vijijini (VMAC). Mafunzo yalitolewa kwa maofisa wahusika katika miundo na miongozo hii mipya kuwawezesha kufanya kazi zao za uratibu kwa ajili ya mwitikio kwenye ngazi za vijiji.
  • Umoja wa Wafanyabiashara Kuhusu UKIMWI Nchini Tanzania ulianzishwa ili kuwezesha kuzidisha programu za UKIMWI zilizopo sehemu za kazi katika asasi binafsi na zile za mchanganyiko nchini. Juhudi kama hizo zilifanywa kuwezesha uanzishwaji wa UMASITA na TIENAI ili kuratibu afua za UKIMWI kwenye sehemu za kazi na sekta isiyo rasmi.
  • Kutokana na kukosekana kwa uwezo na uzoefu katika kuendeleza mwitikio wa UKIMWI katika ngazi ya kitaifa, kimkoa na serikali za mitaa, imeipasa TACAIDS kuchukua majukumu na kufanya kazi nje ya kuwa kiungo cha Mwitikio wa Taifa. Wingi wa kazi na shughuli hizo umezidi idadi ya wafanyakazi katika Tume.