Tovuti ya TACAIDS  inalenga  kusambaza taarifa muhimu za  VVU na UKIMWI kwa jamii, pamoja na kubadilishana uzoefu na wadau wanao tekeleza afua za UKIMWI nchini, ili kuboresha mapambano ya UKIMWI na kufikia malengo yetu ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi ya VVU.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Leonard L. Maboko
MKURUGENZI MTENDAJI

UANZISHAJI WA AFUA MPYA ZA KINGA

Masuala ya Kimkakati Ushahidi kutoka majaribio mawili yaliyofanyika nchini Kenya na Uganda kuhusiana na kutahiri wanaume umeonyesha kuwa hatari ya kuambukizwa kwa virusi vya UKIMWI kwa wanaume ilipungua kwa asilimia hamsini kwa wanaume waliotahiriwa ikilinganishwa na wale ambao hawakutahiriwa. Shirika la Afya Duniani na UNAIDS kwa sasa wanapitia ushahidi huo na kutayarisha miongozo ya kitaalamu kwenye nchi mbalimbali, ikiwemo kivunge cha tathmini ya haraka cha kupima kiwango cha ushamiri wa kutahiri wanaume, kutathmini ukubalifu na kutafuta watu watakaotahiri kwa usalama. Ushamiri wa wanaume waliotahiriwa katika Tanzania ni karibu 70% pakiwepo na tofauti za ushamiri kati ya mikoa na mikoa. Mikoa ya Mbeya na Iringa ambayo ina viwango vikubwa vya ushamiri wa virusi vya UKIMWI na viwango vidogo vya kutahiri wanaume (34.4% Mbeya na 37.7% Iringa), hii inaweza kuashiria uhusiano wa kutahiri na UKIMWI.

Ushauri wa kitaalamu wa wadau unahitaji kufikiria kwa makini vipengele vya sera, mila, haki za binadamu, maadili na uendeshaji vya uhimizaji tohara kwa wanaume. Madhara yanayowezekana kutokea kutokana na kutozingatia taratibu za kutahiri zilizopo na kufanya kitendo hicho kwenye maeneo ambayo siyo safi na kwa kutumia watu wasio na taaluma yanapaswa yatarajiwe na kuepukika. Kulingana na miongozo ya kutoa ushauri nasaha na kupima, suala la kujipima mwenyewe halishauriwi nchini kwetu. Kwa kuwa vivunge vya mtu kujipima vinauzwa kwenye maduka ya dawa ya binafsi, inashauriwa tuanze. kuangalia mahitaji halisi na njia zinazohitajika kuhakikisha kuwa watu wanaotaka kujipima wenyewe wanajua taratibu zinazofaa na matokeo yake na washauriwe ni wapi pa kupata ushauri nasaha, misaada na matunzo