Tovuti ya TACAIDS  inalenga  kusambaza taarifa muhimu za  VVU na UKIMWI kwa jamii, pamoja na kubadilishana uzoefu na wadau wanao tekeleza afua za UKIMWI nchini, ili kuboresha mapambano ya UKIMWI na kufikia malengo yetu ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi ya VVU.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Leonard L. Maboko
MKURUGENZI MTENDAJI

Kupambana na Unyanyapaa, Kujikataa na Ubaguzi:

  • Haki za binadamu za WAVIU na familia zao zinalindwa kwa kutokuwa na tabia ya ubaguzi katika jamii na kupitia upatikanaji ulioboreshwa na huduma rafiki na zinazozingatia jinsia.
  • Uongozi wa ngazi za juu (kisiasa, kimila na kijamii) unakuwepo na kutumika katika shughuli za kupunguza unyanyapaa na kupambana na ubaguzi.