Tovuti ya TACAIDS  inalenga  kusambaza taarifa muhimu za  VVU na UKIMWI kwa jamii, pamoja na kubadilishana uzoefu na wadau wanao tekeleza afua za UKIMWI nchini, ili kuboresha mapambano ya UKIMWI na kufikia malengo yetu ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi ya VVU.

Nyote mnakaribishwa.

Dkt. Leonard L. Maboko
MKURUGENZI MTENDAJI

Uraghibishi na Utashi wa Kisiasa

  • Kudumisha na kuimarisha utashi wa kisiasa, uwazi, uwajibikaji na uungaji mkono na wengi wa afua za VVU kwa kutumia haki za binadamu na mkabala unaozingatia jinsia.
  • Kuongeza uelewa wa wananchi, ukubalifu na ufahamu wa mahitaji na kero za WAVIU pamoja na makundi mengi yaliyo hatarini na yaliyosahauliwa kwa uraghibishi endelevu katika ngazi zote.
  • Kutambua mahitaji maalumu ya makundi mahususi kama vile wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na wale wanaoishi vijijini.
  • Kufanya uchambuzi wa hali halisi ya uraghibishi wa VVU na UKIMWI ili kutambua mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa na changamoto zilizobaki pamoja na upungufu kwa kuzingatia taratibu za uraghibishi zinazofaa na endelevu ikiwemo mikakati itakayozuia unyanyapaa, ubaguzi na kujikataa.