|
Idara/Vitengo na kazi zao |
|
|
IDARA YA URATIBU WA MWITIKIO WA TAIFA
Lengo Kuu Kuratibu shughuli za watekelezaji wote wa masuala ya VVU na UKIMWI nchini Tanzania kupitia miundo iliyopo na kwa kuweka mifumo ya uratibu.
Majukumu
- Kuratibu shughuli zinazolenga kuimarisha mwitikio wa Taifa dhidi ya UKIMWI;
- Kubuni programu za kujenga uwezo na kufuatilia utekelezaji wake;
- Kutoa msaada wa kiufundi kwa watekelezaji wote wa masuala ya VVU na UKIMWI nchini kupitia ngazi ya mkoa;
- Kuratibu shughuli za UKIMWI katika Sekta ya Umma, Sekta Binafsi; Asasi za Kiraia zikiwemo Asasi za Dini, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
- Kujenga uwezo na kuimarisha mitandao mbalimbali na mashirika katika ngazi zote
- Kuangalia shughuli zote zinazopendekezwa na ofisi za Mikoa
IDARA YA URAGHBISHI
Lengo kuu
Kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa mikakati ya uraghibishi kuhusu UKIMWI na wadau wote wa habari zinazohusiana na UKIMWI
Majukumu
- Kuandaa programu za uraghibishi na kufuatilia utekelezaji wake
- Kuratibu shughuli za uraghibishi
- Kutunza, kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka mbalimbali zinazohusu UKIMWI pamoja na kutoa huduma za maktaba kwa wadau na wananchi kwa ujumla.
IDARA YA SERA, MIPANGO NA UTAFITI
Lengo kuu
Kusimamia utekelezaji wa sera na kutoa miongozo ya utekelezaji wa mkakati wa taifa wa kudhibiti UKIMWI na utafiti kuhusu mwitikio wa taifa wa mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI nchini Tanzania.
Majukumu
- Kuandaa mikakati ya utafutaji rasilimali fedha na matumizi yake
- Kufanya utafiti kuhusu VVU/UKIMWI
- Kuhimiza na kuwezesha huduma za sekta binafsi katika Tume
- Kuhakikisha kuwa mipango na bajeti ya VVU/UKIMWI inajumuishwa katika mchakato wa bajeti ya serikali.
Idara hii ina sehemu tatu zifuatazo
KITENGO CHA UFUATILIAJI NA TATHMINI
Lengo Kuu
Kutoa utaalamu na huduma kuhusu ufuatiliaji na tathmini
Majukumu
- Kuandaa mipango ya utekelezaji kuhusu VVU/UKIMWI
- Kuandaa miongozo ya uoanishaji wa mifumo na mbinu za viashirio kwa ajili ya tathmini ya mipango na athari zake.
- Kukusanya na kuchambua data kutoka kwa watekelezaji wa shughuli za VVU/UKIMWI nchini.
- Kuchambua data za VVU/UKIMWI ili ziwe taarifa kwa watumiaji mbalimbali
IDARA YA FEDHA NA UTAWALA
Lengo Kuu Kusimamia na kutoa utalaamu wa masuala yote ya fedha, utumishi na utawala katika Tume
Majukumu
- Kutoa miongozo ya menejimenti ya masuala ya fedha kwa wadau wote wanaoshughulika na VVU na UKIMWI na kufuatilia Utekelezaji wake;
- Kusimamia utoaji wa ruzuku;
- Kusimamia maendeleo ya rasilimali watu
Vitengo vingine ni kama vifuatavyo:
- Kitengo cha Menejimenti ya Mifumo ya Habari
- Kitengo cha Menejimenti ya Manunuzi
- Kitengo ch Ukaguzi wa Ndani
- Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
- Kitengo cha Huduma za Sheria
- Kitengo cha Programu Maalum
|
|
|
Menejimenti |
|
|
Muundo wa Tume |
|
|
Ufuatao ni Muundo wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania
Idara ya Uratibu wa Mwitikio wa Taifa Idara ya Uraghbishi Idara ya Fedha na Utawala Idara ya Sera, Mipango na Utafiti Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Kitengo cha Menejimenti ya Mifumo ya Habari Kitengo cha Menejimenti ya Manunuzi Kitengo ch Ukaguzi wa Ndani Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Kitengo cha Huduma za Sheria Kitengo cha Programu Maalum |
|
|
Uongozi |
|
|
Dira & Dhamira |
|
|
Dira ya TACAIDS ni:
Tanzania inaendeleza juhudi za pamoja za kupunguza kuenea kwa VVU na kutoa matunzo bora zaidi kwa wale walioathirika na walioathiriwa na virusi.
Dhamira ya TACAIDS ni: Kutoa mwongozo na kulinda uongezaji na upanuzi wa ubora wa kinga, matunzo na msaada dhidi ya VVU/UKIMWI na kuwa na ushawishi mkubwa kwenye programu na shughuli mbalimbali za kudhibiti na kupunguza athari ndani ya programu ya mwitikio shirikishi wa Taifa yenye uratibu mzuri unaongozwa na Serikali Kuu, kushikizwa kwenye Halmashauri za Serikali za Mitaa, kujikita ndani ya jamii na kusaidiwa na wadau wote wanaohusika. |
|
|
|
|
<< Start < Prev 1 2 Next > End >>
|
|
Page 1 of 2 |