The Tanzania Commission for AIDS
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Ofisi ya Waziri Mkuu

TUME YA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA
The Tanzania Commission for AIDS | English | 
Home Kuhusu TACAIDS Idara na Vitengo
Idara/Vitengo na kazi zao Print

IDARA YA URATIBU WA MWITIKIO WA TAIFA

Lengo Kuu
Kuratibu shughuli za watekelezaji wote wa masuala ya VVU na UKIMWI nchini Tanzania kupitia miundo iliyopo na kwa kuweka mifumo ya uratibu.

Majukumu

 • Kuratibu shughuli zinazolenga kuimarisha mwitikio wa Taifa dhidi ya UKIMWI;
 • Kubuni programu za kujenga uwezo na kufuatilia utekelezaji wake;
 • Kutoa msaada wa kiufundi kwa watekelezaji wote wa masuala ya VVU na UKIMWI nchini kupitia ngazi ya mkoa;
 • Kuratibu shughuli za UKIMWI katika Sekta ya Umma, Sekta Binafsi; Asasi za Kiraia zikiwemo Asasi za Dini, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
 • Kujenga uwezo na kuimarisha mitandao mbalimbali na mashirika katika ngazi zote
 • Kuangalia shughuli zote zinazopendekezwa na ofisi za Mikoa


IDARA YA URAGHBISHI

Lengo kuu

Kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa mikakati ya uraghibishi kuhusu  UKIMWI  na wadau wote wa habari zinazohusiana na UKIMWI

Majukumu

 • Kuandaa programu za uraghibishi na kufuatilia  utekelezaji wake
 • Kuratibu shughuli za uraghibishi
 • Kutunza, kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka mbalimbali zinazohusu  UKIMWI pamoja na kutoa huduma za maktaba kwa wadau  na wananchi kwa ujumla.


IDARA YA SERA, MIPANGO NA UTAFITI

Lengo kuu


Kusimamia utekelezaji wa sera na kutoa miongozo ya utekelezaji wa mkakati wa taifa wa kudhibiti UKIMWI na utafiti kuhusu mwitikio wa taifa wa mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI nchini Tanzania.

Majukumu

 • Kuandaa mikakati ya utafutaji rasilimali fedha na matumizi yake
 • Kufanya utafiti kuhusu VVU/UKIMWI
 • Kuhimiza na kuwezesha huduma za sekta binafsi katika Tume
 • Kuhakikisha kuwa mipango na bajeti ya VVU/UKIMWI inajumuishwa katika mchakato wa bajeti ya serikali.


Idara hii ina sehemu tatu zifuatazo

 • Sera
 • Mipango na
 • UtafitiKITENGO CHA UFUATILIAJI NA TATHMINI

Lengo Kuu

Kutoa utaalamu na huduma kuhusu ufuatiliaji na tathmini


Majukumu

 • Kuandaa mipango ya utekelezaji kuhusu VVU/UKIMWI
 • Kuandaa miongozo ya uoanishaji wa mifumo na mbinu za viashirio kwa ajili ya tathmini ya mipango na athari zake.
 • Kukusanya na kuchambua data kutoka kwa watekelezaji wa shughuli za VVU/UKIMWI nchini.
 • Kuchambua data za VVU/UKIMWI ili ziwe taarifa kwa watumiaji mbalimbaliIDARA YA FEDHA NA UTAWALA


Lengo Kuu
Kusimamia na kutoa utalaamu wa masuala yote ya fedha, utumishi na utawala katika Tume

Majukumu

 • Kutoa miongozo ya menejimenti ya masuala ya fedha kwa wadau wote wanaoshughulika na VVU na UKIMWI na     kufuatilia Utekelezaji wake;
 • Kusimamia utoaji wa ruzuku;
 • Kusimamia maendeleo ya rasilimali watu


Vitengo vingine ni kama vifuatavyo:

 1. Kitengo cha Menejimenti ya Mifumo ya Habari
 2. Kitengo cha Menejimenti ya Manunuzi
 3. Kitengo ch Ukaguzi wa Ndani
 4. Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
 5. Kitengo cha Huduma za Sheria
 6. Kitengo cha Programu Maalum
 

Idadi ya Warambazaji

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday1
mod_vvisit_counterYesterday99
mod_vvisit_counterThis week608
mod_vvisit_counterLast week721
mod_vvisit_counterThis month525
mod_vvisit_counterLast month3752
mod_vvisit_counterAll days103776

We have: 3 guests, 1 bots online
Today: Feb 06, 2016