|
Zifuatazo ni kazi za TACAIDS: -
- Kutunga miongozo kwa ajili ya mwitikio wa mapambano dhidi ya janga la UKMIWI na usimamizi wa athari zake Tanzania Bara
- Kutayarisha mkakati kwa ajili ya mipango na shughuli za udhibiti wa VVU/UKIMWI kwa mujibu wa mkakati wa Taifa.
-
- Kukuza uhusiano wa kitaifa na kimataifa miongoni mwa wadau wote kupitia uratibu bora wa mipango na shughuli zote za kudhibiti UKIMWI kwa mujibu wa mkakati wa Taifa.
- Kutafuta, kugawa kulingana na mahitaji na kufuatilia matumizi yake.
- Kusambaza na kubadilishana taarifa kuhusu janga la VVU/UKIMWI na madhara yake nchini Tanzania ili tuweze kudhibiti janga hilo.
- Kuhimiza na kuimarisha utafiti, ubadilishanaji taarifa na nyaraka na utunzaji kumbukumbu kwa ajili ya kuzuia na kudhibiti VVU/UKIMWI.
- Kuimarisha program za uraghbishi na elimu kwa kiwango cha juu.
- Kufuatilia na kutathmini shughuli zote za VVU/UKIMWI
- Kuratibu shughuli zote za kudhibiti janga la UKIMWI nchini Tanzania kwa mujibu wa mkakati wa Taifa.
- Kuwezesha juhudi za kupatikana tiba na chanjo na kuimarisha upatikanaji wa huduma na matunzo.
- Kuilinda haki za jamii ya watu walioathiriwa na walioathirika na VVU/UKIMWI
- Kujenga mazingira wezeshi kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI waweze kukubali hali
- Kuishauri serikali kuhusu masuala yote ya udhibiti wa VVU/UKIMWI Tanzania bara.
- Kubainisha vikwazo vya utekelezaji wa afua za VVU/UKIMWI katika sera za kinga, mipango na kuhakikisha ufikiwaji wa malengo yaliyowekwa.
- Kuimarisha shughuli zote zinazohusu huduma za kinga na udhibiti wa janga la UKIMWI katika yafuatayo:
- Huduma za afya na ushauri kwa watu wanao ugua UKIMWI
- Ustawi wa wafiwa, yatima na wategemezi waliobaki.
- Kushughulikia masuala ya kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kisheria yanayohusu janga la UKIMWI
- Kutekeleza shughuli na majukumu mengine yeyote yanayohusu kinga na udhibiti wa UKIMWI katika Tanzania bara kama Tume itakavyoona inafaa.
|