The Tanzania Commission for AIDS
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Ofisi ya Waziri Mkuu

TUME YA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA
The Tanzania Commission for AIDS
TACAIDS
| English | 
Home Matukio Kampeni
Kampeni Print

Uzinduzi wa hivi karibuni wa kampeni ya upimaji wa hiari wa VVU uliofanywa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Julai 2007 unadhihirisha nia thabiti ya Serikali katika kuimarisha mapambano dhidi ya janga hili. Kampeni hii inamtaka kila mtu mzima akapime VVU kwa hiari ili kuhakikisha hali yake ya VVU na kuchukua tahadhari inavyotakiwa dhidi ya maambukizo mapya ya VVU. Kinga dhidi ya maambukizo mapya inawezekana na ndiyo njia pekee ya kudhibiti janga hili. Inasisitizwa kuwa ni jukumu la kila mmoja wetu binafsi na kwa pamoja kuzuia maambukizo mapya ya VVU. Tunawahimiza wazazi, kuhakikisha kuwa kizazi kijacho hakina VVU kwa kujua hali ya VVU ya mama kabla ya kujifungua.