|
Utafiti wa Kiashirio cha VVU/UKIMWI na Malaria Tanzania 2007-08 |
|
|

Hali ya UKIMWI Nchini
Utafiri wa kiashirio cha VVU/UKIMWI na malaria Tanzania 2007-2008 umejumuisha kwa kupima zaidi ya wanawake na wanaume 15,000. Kwa mujibu wa utafiti huo asilimia 5.7 ya watanzania wenye umri wa miaka 15-49 wanamaambukizo ya VVU/UKIMWI.
Maambukizo ya VVU/UKIMWI ni ya kiwango cha juu miongoni mwa wanawake kuliko wanaume katika maeneo ya mijini na vijijini. Wakazi wa mijini ni mara mbili zaidi ya wakazi wa vijijini.
Wanawake wanaambukizwa mapema zaidi kuliko wanaume. Kwa wanawake maambukizo yanaongezeka na umri mpaka inafikia umri wa miaka 30-34 (16.4%). Maambukizo ya kiwango cha juu kwa wanaume yanatokea kati ya miaka 35-39 (10.6%).
Maambukizo ya VVU/UKIMWI Tanzania yamepungua katika miaka ya hivi karibuni. Kiwango cha hivi karibuni cha maambukizo ya VVU/UKIMWI ni 5.7% ambapo 6.6% ni wanawake na 4.6.% ni wanaume. Kwa kulinganisha na utafiti wa kiashirio cha VVU/UKIMWI Tanzania mwaka 2003-2004 (THIS) umebaini maambukizo ya jumla ya VVU/UKIMWI kuwa ni 7%, huku wanawake ikawa 7.7% (6,000) waliopimwa na wanaume 6.3% (4,900) waliopimwa. Matokeo haya yanaonesha kitakimu kushuka kwa maambukizo ya VVU/UKIMWI miongoni mwa wanaume lakini si kwa wanawake.
Maambukizo ya VVU/UKIMWI ni ya juu zaidi katika mkoa wa Iringa (16%), Dar es Salaa na Morogoro (9%) kila mkoa. Kiwango cha maambukizo ni cha chini zaidi Zanzibar ambayo ni chini ya (1%).
Nchini Tanzania maambukizo ya UKIMWI ni ya chini zaidi miongoni mwa wanawake na wanaume wenye elimu ya sekondari au elimu ya juu.
Kwa wanawake na wanaume viwango vya maambukizo ni vya juu zaidi miongoni mwa wajane au walio talikiwa (walioachwa) kuliko wajane au wasio oa au kuolewa au walio oana hivi karibuni. Kati ya wanawake wajane wanne, mmoja ana virusi.
Maambukizo ya VVU/UKIMWI ni ya kiwango cha juu zaidi ni miongoni mwa wanawake na wanaume kwenye kaya zenye kipato kikubwa. Maambukizo ya VVU/UIKIMWI huongezeka kadri ya idadi ya wenza wa ngono inavyoongezeka. Wanawake wenye zaidi ya wenza 10 au zaidi wa ngono wanauwezekano wa mara 7 zaidi wa kuambukizwa VVU/UKIMWI kuliko wanawake wenye mwenza mmoja wa ngono.
Visababishi vya VVU/UKIMWI
Mwenendo na vibainishi vya janga la UKIMWI nchini ni vingi na vinaongozwa na uhusiano wa kingono wa watu wa vipengele vingi vya kijamii, kiutamaduni na kiuchumi. Kwa ujumla, vibainishi vya janga la UKIMWI nchini huenda visitofautiane sana na vile vya sehemu nyingine za Afrika zenye maambukizo ya UKIMWI yaliyoenea nchi nzima. Miongoni mwa vipengele muhimu ni pamoja na vifuatavyo:
- Uasherati
- Matumizi madogo na yasiyo endelevu ya kondomu
- Ngono za marika yanayotofautiana sana
- Kuwa na wapenzi wengi.
- Ukosefu wa elimu ya maambukizo ya UKIMWI
- Kuwepo kwa maradhi mengi ya ngono kama vile tutuko, homa,
- Jando kwa wanaume
Sababu za mahali husika, za kushamiri kwa janga nchini ni:
- Umaskini na biashara ya ngono pamoja na ongezeko la wafanyabiashara wa ngono
- Tabia mbaya za ngono za wanaume kutokana na kuruhusiwa kimila kuwa na nguvu
- Kukosekana usawa wa kijamii, kiuchumi, kisiasa na kijinsia pamoja na unyanyaswaji wa wanawake na wasichana walio ndani na nje ya mahusiano.
- Matumizi ya pombe na dawa za kulevya.
- Tabia za kimila (kama vile utakasaji wajane na jando na unyago)
- Safari za aina zote zinazosababisha kuwa mbali kwa wanandoa na ongezeko la mahawara
- Kutokutahiriwa
|