|
Lengo: Kutunza vielelezo sahihi na jumuisho vilivyotolewa kwa wakati ili kuwezesha kupanga na kufanya maamuzi kuhusu UKIMWI.
Kiashirio: Asilimia ya watekelezaji wa afua za UKIMWI na VVU wanaotoa taarifa za kushiriki katika semina za UKIMWI katika miezi 12 iliyopita.
Masuala ya kimkakati. Ufuatiliaji na Tathmini ni shughuli muhimu katika mipango ya kimkakati. Zinatoa msingi wa kupima matokeo dhidi ya hatua za utekelezaji zilizokusudiwa. Masuala matano ya kimkakati yameathiri kiwango cha kuwepo kwa takwimu kwa ajili ya kupima utendaji uliopita wa mwitikio wa UKIMWI Tanzania:
- Kutokuwepo kwa mazingira wezeshi kwa ajili ya Ufuatiliaji na Tathmini,
- Kutokuwepo uwianishi wa kutosha wa takwimu na mifumo yake,
- Kutokuwepo mtiririko na ukosefu wa kuhakikisha ubora wa takwimu zilizopokewa,
- Matumizi finyu ya takwimu kwa ajili ya kutolea maamuzi
- Kukosekana kwa ajenda zilizoratibiwa.
|