The Tanzania Commission for AIDS
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Ofisi ya Waziri Mkuu

TUME YA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA
The Tanzania Commission for AIDS
TACAIDS
| English | 
Home Nyaraka muhimu
Nyaraka Muhimu
Mipango Mikakati Print

Strategic plans

Mkakati wa Pili wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (2008 – 2012)

Mkakati wa Pili wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NMSF) unahusu kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi 2012. Unaendeleza mafanikio na uwezo wa Mwitikio wa Taifa wa Mapambano dhidi ya UKIMWI katika kipindi cha miaka mitano kilichopita (kuanzia mwaka 2003 hadi 2007) na kupendekeza hatua za kuchukuliwa ikiwemo mikakati ya kukabili vikwazo na matatizo vilivyopita. NMSF huu unaelekeza mikabala, afua na shughuli vitakavyofanywa na watendaji wote nchini. Mkakati huu umetayarishwa baada ya mapitio makubwa na mchakato wa ushauriano chini ya maelekezo ya wataalamu wa Kitaifa na Kimataifa.

Read more...
 
Ripoti Print

Soma Ripoti mbalimbali

 
Takwimu Print

 

Visababishi vya VVU/UKIMWI

Mwenendo na vibainishi vya janga la UKIMWI nchini ni vingi na vinaongozwa na uhusiano wa kingono wa watu wa vipengele vingi vya kijamii, kiutamaduni na kiuchumi. Kwa ujumla, vibainishi vya janga la UKIMWI nchini huenda visitofautiane sana na vile vya sehemu nyingine za Afrika zenye maambukizo ya UKIMWI yaliyoenea nchi nzima.

Miongoni mwa vipengele muhimu ni pamoja na vifuatavyo:

  • Uasherati
  • Matumizi madogo na yasiyo endelevu ya kondomu
  • Ngono za marika yanayotofautiana sana
  • Kuwa na wapenzi wengi.
  • Ukosefu wa elimu ya maambukizo ya UKIMWI
  • Kuwepo kwa maradhi mengi ya ngono kama vile tutuko, homa,
  • Jando kwa wanaume

Sababu za mahali husika, za kushamiri kwa janga nchini ni:

  • Umaskini na biashara ya ngono pamoja na ongezeko la wafanyabiashara wa ngono
  • Tabia mbaya za ngono za wanaume kutokana na kuruhusiwa kimila kuwa na nguvu
  • Kukosekana usawa wa kijamii, kiuchumi, kisiasa na kijinsia pamoja na unyanyaswaji wa wanawake na wasichana walio ndani na nje ya mahusiano.
  • Matumizi ya pombe na dawa za kulevya.
  • Tabia za kimila (kama vile utakasaji wajane na jando na unyago)
  • Safari za aina zote zinazosababisha kuwa mbali kwa wanandoa na ongezeko la mahawara
  • Kutokutahiriwa

 

 
Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI Print

Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI wa mwaka 2008 – 2012 unaendeleza maeneo manne yaliyodhamiriwa ya mkakati wa kwanza na kushughulikia matatizo na upungufu wa miaka iliyopita. Malengo ya Maeneo Yaliyodhamiriwa yamepanuliwa na kuboreshwa ili kutoa mfumo unaofaa kwa ajili ya upangaji wa utekelezaji katika ngazi ya taifa na halmashauri za wilaya kata na vijiji. Ufuatao ni muhtasari wa maeneo yaliyodhamiriwa na malengo ya kimkakati.

 
Sera ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI Print

Sera ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI ilitolewa Septemba 2001