|
Mfuko wa Maendeleo |
|
|
Kufuatia kukamilika kwa mikataba ya Wakala wa Tume wa Mikoa [RFA], TACAIDS imeingia mkataba na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii ili kuendelea kupeleka fedha za MJADU [CARF] kwa Jamii. Aidha mkataba huu ulilenga kukamilisha utoaji wa fedha kutoka mradi wa TMAP amabo unamalizika mwezi Machi 2010 |
|
|
Washirika wa Maendeleo |
|
|
Wafuatao ni baadhi ya Washirika wa Maendeleo wanaoshirikiana na Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI nchini Tanzania:
- Benki ya Dunia
- Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI Kifua Kikuu na Malaria
- Shirika la Misaada la Ubelgiji
- Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti UKIMWI
- Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa
- Mpango wa Chakula Duniani
- Shirika la Afya Duniani
- Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa
- Ubalozi wa Ufaransa
- Idara ya Maendeleo ya Uingereza
- Shirika la Maendeleo la Uswidi
- Shirika la Misaada la Japan
- Shirika la Maendeleo la Canada
- Shirika la Maendeleo la Norway
- Shirika la Maendeleo la Ireland
- Shirika la Maendeleo la Denmark
- Ubalozi wa Falme ya Uholanzi
- Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa
- Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa
- Seikali ya Marekani
- Umoja wa Nchi za Ulaya
- Shirika la Misaada la Ujerumani
- Shirika la Maendeleo la Uswisi
|
|
Asasi za Kiraia (AZAKI) |
|
|
Sekretarieti za Mikoa (RSs) zimepewa jukumu la uratibu, usimamizi na kurahisisha kazi kwenye wilaya na jamii.
Kuundwa kwa Wakala za Uwezeshaji za Mikoa. (RFAs), kila moja ikiwakilisha mikoa miwili ilikuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha msaada wa kiufundi na kifedha unaotolewa wilayani na kwenye jamii. RFAs zinaonekana kama macho, masikio na mikono ya TACAIDS. Ziliweza kuchochea kwa kiasi kikubwa, mwitikio wa wilayani kupitia kujenga uwezo na kuelekeza fedha kwenye CSOs. Pia zimekuwa zikitoa msaada wa kiufundi kwa RSs na CMACs. Hata hivyo RFAs zimekuwa changamoto kubwa katika kufikia na kutoa huduma katika mikoa miwili inayoshughulika nayo. Hili lilikuwa tatizo lililosababisha changamoto kwa upande wa ununuzi na usafirishaji, kudhibiti muda na utoshelevu wa rasilimali. Zaidi ya hayo, kutokana na kwamba RFAs hazikuwa kwenye muundo wa serikali, ilisababisha wakati mwingine kutiliwa shaka na wadau katika ngazi ya mikoa na hivyo kuonekana kama chombo mbadala au pinzani.
|
|
Read more...
|
|
|
TAF |
|
|
Asasi za Kidini |

Kuanzishwa kwa shughuli za UKIMWI wilayani, vijijini, na kata kunahitaji rasilimali endelevu kwa upande wa mafunzo, usimamizi na msaada wa kiufundi. Matumizi ya Kanuni ya Dhana Tatu katika ngazi ya wilaya yameonyesha kuwa changamoto kubwa kwa watendaji wote kutokana na kukosa uzoefu katika mipango shirikishi na uunganishaji pamoja na kuchangia majukumu baina ya sekta mbalimbali. Ushirikishaji wa CSo, katika mipango ya halmashauri unahitaji kuimarishwa, wakati kuaminiana na kusaidiana miongoni mwa watendaji mbalimbali kunahitaji kuendelezwa.
Katika ngazi ya jamii, kuna maelfu kadha ya mashirika ya kijamii (CBOs), pamoja na Mashirika ya Dini (FBos). Hivi vimetoa mchango mkubwa katika Mwitikio wa Taifa, hasa mahali ambapo kulikuwa na fedha na msaada wa kiufundi kupitia asasi zisizo za serikali (AZISE). Nyingi za asasi hizi pia zinajihusisha na ART. Pamoja na idadi yao, uwezo na ubora wa huduma na afua zinazotolewa na CBOs hizo vinatofautiana sana. Uzingatiaji wa miongozo mizuri na ushirikishaji katika jamii pamoja na mipango ya wilaya ni changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi. |
|
|
|
|
<< Start < Prev 1 2 Next > End >>
|
|
Page 1 of 2 |