The Tanzania Commission for AIDS
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Ofisi ya Waziri Mkuu

TUME YA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA
The Tanzania Commission for AIDS
TACAIDS
| English | 
Home Utafiti na Machapisho
Utafiti na Machapisho
Matokeo ya Utafiti Print

Masuala ya kimkakati

Utafiti wa kitabibu na sayansi ya jamii wa UKIMWI unafanyika lakini haujaratibiwa vizuri na hauegemei kwenye ajenda ya utafiti wa UKIMWI uliokubalika kitaifa. Kwa hiyo utafiti unaofanywa unaweza usitoe matokeo hasa yanayokusudiwa. Wakati huohuo utafiti muhimu unakosa fedha. Tatizo jingine ni kwamba utafiti mara nyingi hauendani na mpangilio wa kimkakati wa Mwitikio wa Kitaifa.

Fedha kwa ajili ya utafiti hazitoshelezi na matokeo ya kazi ya utafiti uliyofanyika si mara zote yanasambazwa nchini.

Kuna uelewa finyu wa asili na visababishi vya janga la UKIMWI katika ngazi ya kimkoa na miongoni mwa makundi mbalimbali ya watu. Huduma za UKIMWI ni haba na mara chache zinatolewa kwenye CMAC zote, watekelezaji wa UKIMWI au jamii zilizoathiriwa na utafiti huo. Hali hii imeathiri vibaya uwezo wa CMAC na TACAIDS katika kuratibu mwitikio wa UKIMWI katika ngazi ya wilaya na kitaifa.

Madhumuni ya kimkakati
Kuimarisha uwezo wa kitaifa wa kiutafiti na maendeleo yanayohusu UKIMWI.

Mikakati
1. Kuimarisha uwezo wa wadau na asasi zinazohusika na utafiti wa UKIMWI.
2. Kuimarisha matumizi ya maadili sahihi na pia kusimamia ufuatiliaji wa taratibu halali za kimaadili.
3. Kushughulikia utoaji wa huduma katika ngazi zote ili kuwa na utafiti wa kiutendaji wa UKIMWI.
4. Kanzisha Mkakati wa Taifa wa Utafiti wa UKIMWI na ajenda ya utafiti ambayo imeunganishwa na vipengele muhimu vya NMSF na
5. Kuboresha taratibu za kusambaza matokeo ya utafiti unaohusiana na UKIMWI pamoja na kuzitumia katika kufanya maamuzi.

Kiashirio:
Uwiano wa matokeo kutoka kwenye utafiti wa kitaaluma uliothibitishwa na kamati ya maadili ya kiafya na kisayansi ambayo yamesambazwa katika Tanzania.

 

Matokeo ya Utafiti wa UKIMWI

Kuna idadi ya kutosha ya utafiti wa UKIMWI uliyofanywa nchini na wadau mbalimbali ambao umewasilishwa katika mihadhara ya kitaifa na kimataifa. Hata hivyo utafiti mwingi ni wa kitabibu tu. Hali anuwai za janga la UKIMWI nchini bado hazijaeleweka vizuri kutokana na ukosefu wa takwimu za uchunguzi na utafiti za kijamii, kiuchumi na kitabia. Ajenda ya utafiti wa kitaifa yenye maeneo yaliyofafanuliwa vema ambayo pia habari zake zina changamoto za moja kwa moja za kiutendaji za Mwitikio wa Taifa bado zinakosekana. Usambazaji wa matokeo ya utafiti bado umebakia katika maeneo ya kitaalamu tu kiasi kwamba matumizi yake katika kuwezesha programu za UKIMWI ni finyu sana.

 
Chanjo Print

Chanjo........

 
Vikundi vya Kiufundi Print

Vikundi vya Kiufundi

 
Miongozo ya Utafiti Print

Kwa ujumla hakuna miongozo ya utafiti iliyotayarishwa. Sera ya Taifa ya kudhibit UKIMWI inataja majukumu na njia utafiti zinazoweza kutumiwa na TACAIDS.

 
Kamati ya Taifa ya Ushauri wa Utafiti Print

Kamati ya Taifa ya Ushauri wa Utafiti ina wajumbe kutoka kwenye Wizara, Asasi za Utafiti, Asasi za Elimu ya Juu na Asasi zisizo za kiserikali za Kitaifa na Asasi za Jinsia.


Wajumbe wa  Kamati hiyo wanatoka:

  1. Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OWM-TAMISEMI)
  2. Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS)
  3. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
  4. Wizara ya Sheria na Katiba
  5. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
  6. Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi za Jamii, Muhimbili (MUHAS)
  7. Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)
  8. Chuo cha Maendeleo ya Jamii, Tengeru, Arusha
  9. Mtandao wa Jinsia Tanzania  (TGNP)
  10. Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC)
  11. Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania
  12. Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TDFA)
  13. Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF)
  14. Taasisi ya Utafiti kuhusu Kupunguza Umaskini (REPOA)


Wajumbe wengine wanaweza kualikwa kadri itakavyoonekana inafaa.

 

Majukumu ya Kamati ya Taifa ya Ushauri wa Utafiti

  1. Kubainisha utafiti wa maeneo makuu ya VVU/UKIMWI yanayoweza kufanyiwa kazi kila la mwaka
  2. Kuanzisha mipango mahsusi ya kuharakisha ugharimiaji wa utafiti kuhusu VVU/UKIMWI
  3. Kuhakikisha kuwa upatikanaji wa fedha unafahamika kwa watafiti na kutengwa kwa mujibu wa Ajenda ya Taifa ya Utafiti wa VVU/UKIMWI
  4. Kutoa na kuongoza mfumo wa utafiti wa kitaifa kwa ajili ya utekelezaji, ufuatiliaji na ushirikiano wa shughuli za utafiti wa VVU/UKIMWI
  5. Kutayarisha utaratibu unaoeleweka wa namna ya kuratibu, kufuatilia na kuanzisha uhusiano na asasi za utafiti na kuwa na uelewa wa pamoja
  6. Kusaidia kama za ruzuku za TACAIDS kuhusu aina gani ya utafiti upewe fedha, pia kuweza kujua orodha ya utafiti uliokwishafanywa ili kupunguza kujirudia kwa shughuli miongoni mwa wadau wa utafiti
  7. Kusaidia TACAIDS katika kupitia mapendekezo ya utafiti yaliyopelekwa kwa vyombo vinavyohusika na kuharakisha kuidhinishwa ili kupunguza muda mrefu wa kusubiri kukutana kwa Bodi inayohusika
  8. Kuhimiza na kuimarisha uhusiano vyombo vingine vya utafiti
  9. Kuanzisha orodha na hali ya tafiti zilizofanywa kuhusu VVU/UKIMWI nchini Tanzania kwa manufaa ya watunga sera
  10. Kuanzisha na kuendeleza utaratibu wa uenezaji unaofaa wa matokeo ya utafiti kisanyansi na kwa lugha rahisi inayoelewaka ili kuepuka utata katika kueleweka kwa matokeo ya utafiti kwa Watanzania wa kawaida wanaohitaji kutumia matokeo hayo kwa kuboresha afya na ustawi.