The Tanzania Commission for AIDS
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Ofisi ya Waziri Mkuu

TUME YA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA
The Tanzania Commission for AIDS
TACAIDS
| English | 
Home Utafiti na Machapisho Matokeo ya Utafiti
Matokeo ya Utafiti Print

Masuala ya kimkakati

Utafiti wa kitabibu na sayansi ya jamii wa UKIMWI unafanyika lakini haujaratibiwa vizuri na hauegemei kwenye ajenda ya utafiti wa UKIMWI uliokubalika kitaifa. Kwa hiyo utafiti unaofanywa unaweza usitoe matokeo hasa yanayokusudiwa. Wakati huohuo utafiti muhimu unakosa fedha. Tatizo jingine ni kwamba utafiti mara nyingi hauendani na mpangilio wa kimkakati wa Mwitikio wa Kitaifa.

Fedha kwa ajili ya utafiti hazitoshelezi na matokeo ya kazi ya utafiti uliyofanyika si mara zote yanasambazwa nchini.

Kuna uelewa finyu wa asili na visababishi vya janga la UKIMWI katika ngazi ya kimkoa na miongoni mwa makundi mbalimbali ya watu. Huduma za UKIMWI ni haba na mara chache zinatolewa kwenye CMAC zote, watekelezaji wa UKIMWI au jamii zilizoathiriwa na utafiti huo. Hali hii imeathiri vibaya uwezo wa CMAC na TACAIDS katika kuratibu mwitikio wa UKIMWI katika ngazi ya wilaya na kitaifa.

Madhumuni ya kimkakati
Kuimarisha uwezo wa kitaifa wa kiutafiti na maendeleo yanayohusu UKIMWI.

Mikakati
1. Kuimarisha uwezo wa wadau na asasi zinazohusika na utafiti wa UKIMWI.
2. Kuimarisha matumizi ya maadili sahihi na pia kusimamia ufuatiliaji wa taratibu halali za kimaadili.
3. Kushughulikia utoaji wa huduma katika ngazi zote ili kuwa na utafiti wa kiutendaji wa UKIMWI.
4. Kanzisha Mkakati wa Taifa wa Utafiti wa UKIMWI na ajenda ya utafiti ambayo imeunganishwa na vipengele muhimu vya NMSF na
5. Kuboresha taratibu za kusambaza matokeo ya utafiti unaohusiana na UKIMWI pamoja na kuzitumia katika kufanya maamuzi.

Kiashirio:
Uwiano wa matokeo kutoka kwenye utafiti wa kitaaluma uliothibitishwa na kamati ya maadili ya kiafya na kisayansi ambayo yamesambazwa katika Tanzania.

 

Matokeo ya Utafiti wa UKIMWI

Kuna idadi ya kutosha ya utafiti wa UKIMWI uliyofanywa nchini na wadau mbalimbali ambao umewasilishwa katika mihadhara ya kitaifa na kimataifa. Hata hivyo utafiti mwingi ni wa kitabibu tu. Hali anuwai za janga la UKIMWI nchini bado hazijaeleweka vizuri kutokana na ukosefu wa takwimu za uchunguzi na utafiti za kijamii, kiuchumi na kitabia. Ajenda ya utafiti wa kitaifa yenye maeneo yaliyofafanuliwa vema ambayo pia habari zake zina changamoto za moja kwa moja za kiutendaji za Mwitikio wa Taifa bado zinakosekana. Usambazaji wa matokeo ya utafiti bado umebakia katika maeneo ya kitaalamu tu kiasi kwamba matumizi yake katika kuwezesha programu za UKIMWI ni finyu sana.