The Tanzania Commission for AIDS
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Ofisi ya Waziri Mkuu

TUME YA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA
The Tanzania Commission for AIDS
TACAIDS
English | Kiswahili 
Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI Print

Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI wa mwaka 2008 – 2012 unaendeleza maeneo manne yaliyodhamiriwa ya mkakati wa kwanza na kushughulikia matatizo na upungufu wa miaka iliyopita. Malengo ya Maeneo Yaliyodhamiriwa yamepanuliwa na kuboreshwa ili kutoa mfumo unaofaa kwa ajili ya upangaji wa utekelezaji katika ngazi ya taifa na halmashauri za wilaya kata na vijiji. Ufuatao ni muhtasari wa maeneo yaliyodhamiriwa na malengo ya kimkakati.