News
RAS ARUSHA ATAKA MPANGO WA PAMOJA WA KINGA YA VVU KUELEKEA MICHUANO YA AFCON 2027
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt. Toba Alnason Nguvila, amesisitiza umuhimu wa kuwa na mpango mmoja wa pamoja unaowashirikisha Serikali, TACAIDS, Halmashauri, sekta ya afya, sekta binafsi, Asasi za kiraia, washirika wa maendeleo, Sekta ya Utalii, vyombo vya habari na wadau wa michezo katika maandalizi ya AFCON 2027, hususan katika kuimarisha kinga dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) Mkoani Arusha

