News
TACAIDS NA WHO ZAKUBALIANA KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA MWITIKIO WA UKIMWI
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Catherine Joachim mapema Leo tarehe 20 Mei, 2025 amekutana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tanzania, Dkt Charles Sagoe - Moses jijini Dar es salaam. Katika mazungumzo wamejadili masuala yanayolenga uimarishaji wa huduma jumuishi za mwitikio wa UKIMWI nchini.
Dkt Catherine alisema, Mafanikio yaliyofikiwa na Tanzania katika kupunguza maambukizi mapya ya VVU na vifo vitokanavyo na UKIMWI yametokana na uwepo wa Sera, Mikakati na Miongozo madhubuti iliyoandaliwa na Serikali kwa kushirikiana na Wadau wakiwemo WHO.
Kwa upande wa Dkt. Charles alisisitiza kwamba "WHO itaendelea kushirikiana na TACAIDS kwa kutoa ushauri wa kitaalam ili kuhakikisha malengo ya viashiria vya kitaifa vya mwenendo wa UKIMWI vinafikiwa ifikapo 2030.