Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania
The Prime Minister's Office

Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

News

KAMATI YA UKAGUZI YA TACAIDS YASISITIZA UWAZI NA UWAJIBIKAJI


Kamati ya Ukaguzi ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imefanya kikao chake cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/2026, ambapo imeweza kujadili taarifa muhimu ikiwemo taarifa ya mapato na matumizi kwa robo ya kwanza, taarifa ya manunuzi, mpango wa mwaka wa ukaguzi wa ndani pamoja na taarifa za mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF). Kamati hii ni moja ya mifumo inayohakikisha uwepo wa uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI nchini.