Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania
The Prime Minister's Office

Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

News

TACAIDS YATOA MAFUNZO YA VVU NA UKIMWI KWA VIJANA WILAYA YA CHAMWINO


Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania-TACAIDS kwa kushirikiana na wadau na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imetoa mafunzo kwa vijana wa kata ya Dabalo wilayani Chamwino kuhusu kujikinga na VVU na UKIMWI, matumizi sahihi ya Kondom, kupinga Unyanyapaa na Ubaguzi kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) pamoja na kukinga maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na elimu kuhusu Mwitikio wa UKIMWI nchini.

Mafunzo hayo yametolewa kwa lengo la kuwaongezea vijana uelewa katika masuala muhimu ya VVU na UKIMWI ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana kuzifikia huduma za UKIMWI kama vilw upimaji,huduma za Kinga, Matibabu na Matunzo ili kufikia malengo ya kutokomeza UKIMWI kama tishio la afya ya jamii ifikapo mwaka 2030.