News
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALA YA UKIMWI YAPITISHA MAKADIRIO YA MPANGO WA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2026/2027
Na Mwandishi wetu- Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imepitisha makadirio ya mpango na bajeti ya shilingi Bilioni 12, 681, 254, 681 ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Bajeti hiyo imewasilishwa leo tarehe 26 Machi 2026, na Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma ambapo pia amewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Mara baada ya kujadiliwa na kupitishwa na wajumbe, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dkt. Johannes Lukumay ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyohakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi katika maeneo mbalimbali.
Vilevile, Mhe. Dkt. Lukumay ameeleza kuwa, Serikali imewekeza nguvu kubwa katika nyanja ya afya kwa kuboresha miundombinu ya afya kwani ndiyo mtaji wa maendeleo.
Aidha, Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa ameahidi kufanyia kazi ushauri na maoni yaliyotolewa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ili sekta hiyo muhimu iwe imara na yenye matokeo chanya kwa wananchi katika maeneo yote nchini.

