News
MKURUGENZI MTENDAJI AMEFANYA KIKAO KAZI NA WATUMISHI WA TACAIDS
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS Dkt. Adam Joseph Mrisho amefanya kikao Kazi cha kwanza na watumishi wa TACAIDS.
Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Mrisho ametoa shukrani kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua katika nafasi ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS.
Aidha, ametoa hamasa ya uwajibikaji na kujituma kwa watumishi wa TACAIDS na kusisitiza kufanya kazi kwa ushirikiano.
Kwa upande wake aliekua Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Samwel Sumba naye ametoa shukrani kwa watumishi wa TACAIDS kwa ushirikiano waliompa katika kipindi cha uongozi wake.

