News
TACAIDS NA UNI-AWARDS WAWAFIKIA VIJANA WA VYUO KUTOA ELIMU YA VVU NA UKIMWI
Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kwa kushirikiana na UNFPA na Uni-Awards imeendelea kuimarisha jitihada za mwitikio wa VVU na UKIMWI kwa kutoa elimu kwa vijana wa vyuo vikuu na kati. Katika mkutano uliofanyika Juni 2, 2026 katika chuo cha City College of Health Sciences, Temeke jijini Dar es Salaam ambapo wanafunzi walipata mafunzo kuhusu mwitikio wa UKIMWI, ikiwemo kupinga unyanyapaa na ubaguzi, huduma za kinga, upimaji, matibabu na matunzo ya VVU.
Lengo kuu la kampeni hii ni kuwawezesha vijana kupata taarifa sahihi za afya, kuongeza uelewa wao na kuhamasisha ushiriki katika mapambano ya kitaifa dhidi ya UKIMWI. Vijana wanachukuliwa kama nguzo muhimu katika kufanikisha malengo ya kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030.
Kwa kushirikiana na wadau, TACAIDS inaendelea kuhakikisha kila kijana anapata elimu, huduma na msaada unaohitajika ili kujenga jamii yenye afya bora na yenye usawa.

