Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania
The Prime Minister's Office

Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

News

​TACAIDS yaongoza kikao kazi cha Wadau wa Mradi wa DREAMS


Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imeongoza kikao cha wadau wa mradi wa DREAMS kujadili namna bora ya utekelezaji wa mradi huo. Kikao hicho kimefanyika Leo Februari 3, 2025 jijini Dodoma kwa kuwaleta pamoja wadau kutoka Wizara za kisekta.

Aidha, Mradi wa DREAMS ambao ulilenga kusaidia vijana wa kike walioko kwenye mazingira hatarishi, umeonyesha mafanikio makubwa katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Shinyanga, Kagera na Mwanza. Kupitia ushirikiano wa Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI, TACAIDS, Wizara ya Afya na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, mradi umeweza kutoa fursa za elimu, afya na ulinzi wa kijamii kwa mabinti wadogo.

Vile vile, Serikali kupitia TACAIDS imejipanga kuhakikisha Vijana wanafikiwa na Huduma kwa ujumla. Uwekezaji katika vijana wa kike ni msingi wa kupunguza maambukizi mapya ya VVU na kuimarisha ustawi wa jamii.

Kikao hicho kilihitimishwa kwa wito kuhakikisha programu za vijana zinaendelea kuwa nguzo ya matumaini kwa mabinti wa Kitanzania.