Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania
The Prime Minister's Office

Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

News

BODI YA ATF YAJIONEA UTEKELEZEJI WA AFUA MBALIMBALI DHIDI YA VVU NA UKIMWI


Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (AIDS Trust Fund-ATF) Bw. Sabasaba Moshingi amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Mkoa wa Geita katika kuimarisha Mwitikio wa VVU na UKIMWI kwa lengo la kupunguza Maambukizi mapya ya VVU kwenye mkoa huo

Bw Moshingi ametoa pongezi hizo wakati wa ziara katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Katika ziara hiyo wajumbe wameelezwa taarifa ya mwenendo wa UKIMWI mkoani Geita na utekelezaji wa huduma za kinga, matibabu na matunzo na Kujadili umuhimu wa kuendelea kuimarisha utoaji wa elimu na huduma za kinga dhidi ya VVU, hususan kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya machimbo, na maeneo ya maegesho ya magari ya mizigo katika mkoa huo.