Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania
The Prime Minister's Office

Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

News

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALA YA UKIMWI YAPITISHA BAJETI YA TACAIDS


Na Mwandishi wetu- DODOMA

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Mhe. Dkt Christina Mnzava ameipongeza Serikali kwa kuongeza bajeti katika Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF) ili kuendelea kusimamia Afua kwa kutumia fedha za ndani.

Dkt. Mnzava amesema hayo leo tarehe 24 Machi, 2025 jiji Dodoma wakati wa kupitishwa taarifa ya utekelezaji wa mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024-2025 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2025-2026 kwa fungu 92 Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) inayofanya majuku yake chini ua Ofisi ya Waziri Mkuu

“Nimpongeze Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuongeza fedha katika mfuko wetu ni hatua nzuri sana, niwasihi watendaji wa Serikali kuendelea kufuatilia fedha hizi ili mipango tuliojiwekea iweze kutekelezwa kwa usahihi,” Alisema Dkt. Mnzava.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Willliam Lukuvi alibainisha kwamba kulingana na hali ya sasa ya usitishwaji wa misaada kutoka fedha za nje, serikali imejipanga kuendelea kutekeleza AFUA muhimu zenye tija na kuleta matokeo makubwa ifikapo mwaka 2030.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania Dkt. Catherine Joachim amesema tume ilidhinishiwa muundo mpya ambao ulifanya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Kuwa na Vitengo saba na Ofisi za kanda saba .

Aidha alieleza kwamba ili kuimarisha uratibu Mameneja wa Kanda ambao wako chini ya Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa watajengewa uwezo ili waweze kutembelea mikoa ambayo wanairatibu.