News
TACAIDS YAPANUA WIGO WA UTOAJI ELIMU YA VVU NA UKIMWI KUPITIA MAONESHO YA 12 YA ZITF
Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imetumia fursa ya maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Zanzibar (Zanzibar International Trade Fair - ZITF) kutoa elimu ya VVU na UKIMWI. Kupitia Monesho ya Biashara za kimataifa za Zanzibar -ZITF (Zanzibar International Trade Fair)
Maonesho hayo ya 12 yanafanyika viwanja vya Dimani Mkoani Magharibi kisiwani Unguja ambapo yamehudhuriwa na wadau kutoka ndani na nje ya Nchi.
Elimu hiyo ya VVU na UKIMWI inalenga kuwasaidia Wananchi kujikinga na Maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI, kuondoa unyanyapaa na ubaguzi kwa Watu Wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI (WAVIU), kuhamasisha matumizi ya kipimo cha upimaji wa VVU binafsi cha Jipime na kuhamasisha ufuasi mzuri wa huduma za tiba na matunzo kwa WAVIU.

