News
TACAIDS yashiriki Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha
Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imeendelea kuelimisha wananchi kwa kushiriki katika maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyofanyika jijini Tanga, chini ya kauli mbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii.”
Maonesho hayo yamezinduliwa rasmi na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Deogratius Luswetula, Januari 21, 2026 jijini Tanga na yameshirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya fedha na maendeleo ya Jamii. Katika maonesho hayo, TACAIDS imeweka mkazo wa kuhamasisha wananchi kutumia huduma za VVU na UKIMWI pamoja nae limu ya kujikinga na maambukizi ya VVU na kuimarisha mwitikio wa UKIMWI nchini.
Kupitia maonesho haya, TACAIDS imeonesha dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuimarisha afya ya jamii, ikisisitiza kuwa elimu ya fedha na afya ni nguzo muhimu za ustawi wa kijamii na kiuchumi.

