Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania
The Prime Minister's Office

Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

News

Kampeni ya furaha yangu kurejeshwa ili kuongeza hamasa kwa wanaume kupima Afya zao.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amewasilisha Utekelezaji wa Mpango wa bajeti na bajeti ya mwaka 2023/24 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 ya Tume ya udhibiti UKIMWI Tanzania kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI,walipokea na kuijadili, tarehe 21Machi,2024 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Wakijadili Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 ya Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania, kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, iliipongeza TACAIDS kwa kazi ambayo wameifanya katika Mapambano ya VVU na UKIMWI.

Aidha wamesema pamoja kazi kubwa ambayo tayari imefanyika bado jitihada zaidi zinahityajika kuhamasisha wanaume kupima Afya kwani bado Taarifa ya Vaishiria vya UKIMWI ya mwaka 2022/23 inaonesha hali ya upimaji wa wanaume bado hairidhishi,na kushauri kurejesha Kampeni ya Furaha yangu ili kuendelea kuhamasisha wanaume kupima.

Kamati iliagiza TACAIDS kubuni miradi ambayo itawashirikisha wanaume ili kuwainua kiuchumi kupitia miradi wanayoiratibu ambayo inatekelezwa na wadau, kwakuwa miradi mingi ambayo wamekuwa wakitembelea wamekuta ni wanawake tu ndio wanaofanya miradi.

Awali Mhe Jenista alimshukuru mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI kwa kuendelea kuishauri serikali katika masuala ya UKIMWI na Afya kwa ujumla na kuwashukuru wajumbe wa kamati hiyo kwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakiifanya, maoni na ushauri wao ambao umekuwa ukisaidia katika kuongoza mapambano dhidi ya UKIMWI nchini.