News
KATIBU MKUU DKT. JIM YONAZI ATEMBELEA KITUO CHA MAARIFA KAZURAMIMBA MKOANI KIGOMA KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA VVU NA UKIMWI
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera , Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania- TACAIDS, Dkt. Adam Mrisho wametembelea Kituo cha Maarifa Kata ya Kazuramimba, Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma na kukutana na vijana wanaotekeleza afua za VVU na UKIMWI kupitia vikundi. Dkt. Jim Yonazi na Dkt. Adam Mrisho wamewapongeza vijana hao kwa kazi nzuri wanayoifanya na kusisitiza kuwawezesha kiuchumi na akuwajengea uwezo kaika kuimarisha mwitikio dhidi ya VVU na UKIMWI.

