News
KATIBU MKUU DKT. JIM YONAZI ATEMBELEA OFISI YA MKOA WA SHINYANGA KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA VVU NA UKIMWI
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera , Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania- TACAIDS, Dkt. Adam Mrisho wametembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kukutana na Mkuu wa Mkoa Mhe. Mboni Mhita ambapo walijadili juhudi za Mkoa huo katika kuimarisha huduma za upimaji wa VVU na kinga dhidi ya VVU na UKIMWI. Mhe Mboni Mhita alieleza juhudi zinazofanywa katika kupunguza maambukizi mapya na kuimarisha mwitikio dhidi ya VVU na UKIMWI

