News
KIKAO CHA KAMATI NDOGO YA KITAIFA YA KONDOM
Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania - TACAIDS imeratibu Kikao cha Pili cha Robo ya Mwaka cha Kamati Ndogo ya Kitaifa ya Kondomu kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Kikao hicho kimefanyika Januari 8, 2026 Jijini Dodoma na kuwaleta pamoja wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa Serikali, Mashirika binafsi na washirika wa maendeleo kujadili utekelezaji wa mikakati ya kitaifa ya upatikanaji na matumizi salama ya kondomu.
Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni Mapitio ya utekelezaji wa mpango wa robo ya kwanza, Uwepo wa mashine za ugawaji wa kondomu katika maeneo nyenye vichocheo vya maambukizi ya VVU, Mikakati ya kuongeza upatikanaji wa kondomu katika maeneo ya vijijini na mijini pamoja na Uhamasishaji wa jamii na vijana kuhusu matumizi sahihi ya kondomu kama njia ya kinga dhidi ya VVU na magonjwa ya zinaa. Ushirikiano huu wa kisekta ili kuhakikisha uendelevu wa huduma na kampeni za kitaifa.
Kamati imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha malengo ya kitaifa ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU na kulinda afya ya jamii yanafikiwa.

