News
MKUTANO WA USAMBAZAJI WA TAARIFA YA MAPITIO YA FEDHA ZA UKIMWI
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS)
Dkt.Leonard Maboko amesema jitihada za ziada zinahitajika katika
kuimarisha vyanzo vya ndani vya fedha za kupambana UKIMWI nchini.
Akizungumza wakati wa kufunga kikao cha waratibu wa UKIMWI kutoka
Wizara, Mikoa na Halmashauri kilichofanyika Mkoani Singida cha usambazaji
wa taarifa ya mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya
mwaka 2022
Dkt. Maboko alisema fedha za UKIMWI zinazidi kupungua kwa asilimia 15
mwaka hadi mwaka, hivyo kuwa jitihada za ziada zinahitajika katika
kuimarisha vyanzo vya ndani.
Hadi sasa fedha nyingi zinategemewa katika Mwitikio wa UKIMWI ni zile
zinazotoka kwa wadau wa maendeleo bado hatujafikia pazuri katika vyanzo
vyetu vya ndani (domestic financing) na hata fedha inayopangwa katika
lengo A katika bajeti ya Mwaka katika Wizara na taasisi za Umma
haipatikani ili kutekeleza Malengo yaliyokusudiwa.
Changamoto ni kuwa kama nchi bado hatujaweza kujitegemea wenyewe
katika Mwitikio wa VVU na UKIMWI, licha ya malengo yaliyopo ya kufikia
2030 kuwa kama nchi tuwe tumefikia sifuri tatu, maambukizi mapya sifuri,
vifo viwe vimefikia sifuri na unyanyapaa uwe umefikia sifuri.
Dkt. Maboko alisisitiza kuwa ni kweli kuwa fedha kutoka kwa wafadhili
zinapungua katika miaka miaka 2 hadi mitatu ya nyuma na mwelekeo wa
wa miaka ijayo kupitia vikoa vya watalaamu na wadau wa maendeleo
fedha za mwitikio wa VVU na UKIMWI zinaendelelea kupungua kwa silimia
15.
Aidha wakati wa kongamano la kimataifa la UKIMWI lililofanyika nchini
Canada Mkurugenzi wa UNAIDS Duniani alisema katika miaka3- 5 ijayo
mabilioni ya fedha za UKIMWI zitapungua na hili sio suala la Tanzania
pekee ni changamoto ya nchi zote.
“sasa lazima tuimarishe vyanzo vya fedha za ndani,kwani malengo yapo
pale pale na hatujayafikia na maambukizi mapya kwa mwaka watu 54,000
wanapata maambukizi ya VVU, hii ukichukulia kwa siku watu 147 wanapata
maambukizi mapya, ambapo mwaka 2007 watu 200 walikuwa wanapata
maambukizi mapya.
Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 30 ni kwa vijana wa miaka 15 hadi
24, ambapo kwa siku vijana 44 wanapata maambukizi ya VVU, wakati huo
takwimu zinaonesha vijana wa kike 31 wanapata maambukizi ya VVU kwa
siku kupitia takwimu hizi ni wazi kuwa kuna haja ya kuweka nguvu na
raslimali nyingi kwa vijana.
Miradi ya vijana kwa kutegemea wafadhili yaani PEPFAR tupo katika
halamshauri 11 lakini kwenye mipango ya mwaka huu zitafika halmashuri
14 kupitia mradi wa Dreams, wakati Global fund ni halmashauri 18
zilizofikiwa kwahiyo hadi sasa ni halmashauri 32 kati ya halmashauri 187.
Pamoja na upungufu uliopo bado hatujafikia halmashauri zote nchini
kwahiyo ni muhimu, tunapopanga mipango yetu vipaumbele viwe kwa
maeneo ambayo hayajafiwa na wafadhili.