Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania
The Prime Minister's Office

Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

News

​TACAIDS NA ILO KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA VVU NA UKIMWI MAHALA PA KAZI


Utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI mahala pa kazi umetajwa kuwa ni moja ya njia bunifu za kufikisha huduma za VVU na UKIMWI maeneo ya kazi kwa watumishi na jamii inayowazunguka.

Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Catherine Joachim na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) nchini Bi. Caroline Khamati Mugalla. Dkt. Catherine alisema, anawashukuru ILO kwa mchango wao katika utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI zinazolenga kutokomeza unyanyapaa wa masuala ya VVU/UKIMWI.

Kwa upande wa ILO. Bi Caroline ameipongeza TACAIDS kwa uratibu na utoaji wa miongozo bora inayowasaidia wadau wengi ikiwemo ILO katika kutekeleza afua za VVU na UKIMWI mahala pa kazi. Aidha, Bi. Caroline amesisitiza kuwa wataendelea kuhakikisha vyama vya Wafanyakazi pamoja na TACAIDS wanakuwa na jukwaa la mijadala ya pamoja ili kuhakikisha vyama hivyo vinakua na mchango katika kutokomeza maambukizi ya VVU pamoja na unyanyapaa na ubaguzi kwa WAVIU mahala pa kazi hapa nchini