Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania
The Prime Minister's Office

Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

News

TACAIDS NA UNAIDS WAKUBALIANA KUIMARISHA URAGHIBISHI KATIKA MWITIKIO WA UKIMWI


Dar es salaam,

Wakati Tanzania ikiendelea kujivunia mafanikio yaliyofikiwa katika mwitikio wa UKIMWI ikiwa ni pamoja na kupungua kwa maambukizi mapya kutoka watu 72,000 kwa mwaka kulingana na takwimu za mwaka 2016/17 hadi watu 60,000 kwa mwaka kulingana na takwimu za mwaka 2022/23.

Mafanikio hayo na mengine mengi yamebainishwa wakati Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Catherine Joachim alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI (UNAIDS) jijini Dar es salaam Leo tarehe 20 Mei, 2025.

Akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika hilo Dkt. Martin Odiit, Dkt. Catherine alisema serikali inaendelea kujivunia ushiriki wa wadau wa maendeleo ikiwemo UNAIDS katika kuhakikisha malengo ya kutokomeza UKIMWI yanafikiwa.

Aidha Dkt. Odiit alisisitiza kwamba UNAIDS ipo tayari kuendelea kushirikiana na serikali katika kupambana na VVU na UKIMWI ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa kitaalamu kwenye mambo mbalimbali ikiwemo ya kuimarisha uraghibishi na kuongeza rasilimali za ndani kwa ajili ya mwitikio wa UKIMWI.