Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania
The Prime Minister's Office

Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

News

TACAIDS YAWASILISHA TAARIFA YA UTENDAJI KAZI KWENYE KAMATI YA BUNGE


Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imewasilisha taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Disemba, 2024 kwenye kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshugulikia masuala ya Afya na UKIMWI. Katika mawasilisho yake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Catherine Joachim alieleza kamati kwamba pamoja na changamoto za upatikana ji wa rasilimali za UKIMWI nchini bado TACAIDS imeweza kutekeleza shughuli zinazolenga kukuza mwitikio wa UKIMWI nchini.

Shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na zile zilizolenga kuwezesha vikundi vya WAVIU, kuimarisha huduma za kinga pamoja na kuhamasisha mabadiliko ya tabia hatarishi zinazochochea maambukizi ya VVU. Akizungumza kuhusu hali ya maambukizi ya VVU nchini, Dkt. Catherine alisisitiza kwamba kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU bado ni kikubwa kwa vijana hasa vijana wakike. Kwa upande wa maambukizi mapya alieleza kwamba kwa mwaka inakadiriwa kuwa watu 60000 wanaambukizwa VVU ambapo kwa siku ni takribani watu 164. “TACAIDS inaendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa jamii, kuimarisha uratibu pamoja na kuendelea kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI ili kufikia malengo ya kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030” alisema Dkt. Catherine

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na UKIMWI Mhe. Elibariki Kingu aliwashukuru TACAIDS kwa jitihada wanazozifanya na akasisitiza uratibu kwa sekta binafsi uimarishwe ili wadau walio katika sekta hiyo waweze kuchangia kwenye mwitikio wa UKIMWI hapa nchini