Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania
The Prime Minister's Office

Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

News

TACAIDS YAWEKA MIKAKATI MADHUBUTI KATIKA MWITIKIO DHIDI YA VVU NA UKIMWI


Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania- TACAIDS inaendelea kuimarisha mikakati madhubuti ya mwitikio dhidi ya VVU na UKIMWI kupitia ushirikiano wa kısekta, kuhamasisha vyanzo vya fedha vya ndani ili kuongeza huduma karibu katika jamii ikiwemo Vituo vya Maarifa kwa madereva wa malori na kuwajengea uwezo wanawake na vijana ili kufikia lengo la kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030. Ameyabainisha hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI