Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania
The Prime Minister's Office

Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

News

​TAMATI ZA MWENGE WA UHURU KUSISITIZA MAPAMBANO DHIDI YA VIRUSI VYA UKIMWI


Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 zimefikia tamati kwa kutoa msisitizo juu ya utoaji wa elimu na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI nchini

Msisitizo huo umetolewa leo Oktober 14,2025 na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Comrade Ismail Ali Ussi wakati akisoma lisala ya kutamatisha mbio na kukabidhi rasmi Mwenge wa Uhuru kwa Mhe Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango katika viwanja Sokoine jijini Mbeya.

"Pamoja na Ujumbe mkuu Mwenge wa UHURU umeendelea kusisitiza mapambano dhidi ya Rushwa, Mapambano dhidi ya UKIMWI, Mapambano dhidi ya dawa zakulevye na elimu juu ya Lishe" alisema Comrade Ismail Ussi

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS Dkt Samwel Sumba ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia mapambano dhidi ya UKIMWI kupitia Bajeti ya mwaka wa fedha 2025-2026.

Sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru zilizoambatana na maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa zimetamatishwa kwa kubeba Ujumbe maalumu uliosema "Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa amani na Utulivu"