News
TANZANIA KUWEKA MKAKATI MADHUBUTI KUKABILI VVU NA UKIMWI KWA USHIRIKIANO WA KIKANDA
Tanzania imechukua hatua muhimu katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI Kwa kushirikiana na mashirika, taasisi pamoja na sekta mbalimbali kujadili Mkakati wa utekelezaji wa Huduma za kinga.
Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya UKIMWI (UNAIDS) pamoja na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP) wamejadili Mkakati wa Huduma za kinga dhidi ya VVU na UKIMWI wa Mwaka 2024 - 2030 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Kikao Kazi hicho kimefunguliwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Samwel Sumba Leo Septemba 18, 2025 jijini Dar es Salaam.